iqna

IQNA

Mashahidi
IQNA - Waziri wa Utamaduni wa Lebanon amesema hayati Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje i Hossein Amir-Abdollahian, ambao walikufa shahidi katika ajali ya hivi majuzi ya helikopta, walisimama na watu wa Palestina kwa misimamo madhubuti.
Habari ID: 3478917    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/06/02

Kufa Shahidi Rais wa Iran na Wenzake
IQNA-Kituo cha Mawasiliano cha Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimechapisha ripoti ya pili ya Kamisheni Kuu ya kuchunguza sababu za ajali ya helikopta ya shahidi Rais Seyed Ebrahim Raisi, na ujumbe ulioandamana nao.
Habari ID: 3478900    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/29

IQNA-Bango la "Sauti ya Watoto wanaodhulumiwa wa Palestina" limesambazwa ili kuenzi juhudi za shahidi Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watu wanaodhulumiwa wa Palestina hasa watoto katika vikao na taasisi za kimataifa.
Habari ID: 3478894    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/28

Maombolezo
IQNA - Qari mashuhuri wa Iran Ustadh Karim Mansouri alisoma aya ya 100 ya Surah An-Nisa na vile vile aya za mwisho za Surah Al-Fajr katika kikao cha Khitma ya Qur'ani kwa ajili ya hayati shahidi Rais Ebrahim Raisi wa Iran na mashahidi wenzake.
Habari ID: 3478889    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/26

Ulimwengu wa Kiislamu
IQNA - Mwanazuoni wa Lebanon anasema kufa shahidi Rais wa Iran hayati Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian ilikuwa hasara kwa Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3478888    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/26

Maombolezo
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mahuhudurio makubwa ya wananchi Waislamu wa Iran kwenye mazishi na misafara ya kuwaaga na kuwaenzi Rais Ebrahim Raisi wa Iran na mashahidi wenzake yameidhihirishia dunia kuwa, Wairani ni waaminifu na wamefungamana na nara za Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3478884    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/25

Maombolezo
IQNA-Waislamu nchini Tanzania wameshiriki katika kikao cha kumuomboleza na kumuenzi Shahidi Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyekufa shahidi Jumapili iliyopita katika ajali ya helikopta akiwa na wenzake akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian.
Habari ID: 3478883    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/25

Maombolezo
IQNA-Mwili wa Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita kaskazini magharibi mwa nchi umezikwa leo katika Haram ya Shah Abdul Adhim Hassani (AS) katika mji wa Shahre-Rey, eneo la kusini la makoa wa Tehran.
Habari ID: 3478877    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/23

Maombolezo
IQNA-Kufuatia kufa shahidi Rais Ebrahim Raisi wa Iran na wenzake katika ajali ya helikopta, Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammad Shia al-Sudani, amefika Tehran na kukutana na Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kumpa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali na taifa la Iraq.
Habari ID: 3478875    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/23

Diplomasia ya Kiislamu
IQNA-Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo na Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas na ujumbe alioandamana nao kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kutokomezwa utawala wa Kizayuni itatimia.
Habari ID: 3478874    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/23

Maombolezo
IQNA-Viongozi na maafisa wakuu wa nchi 68 duniani leo wamefika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Tehran kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Rais Sayyid Ebrahim Raisi na ya wenzake waliokufa shahidi pamoja naye katika ajali ya helikopta iliyotokea siku ya Jumapili.
Habari ID: 3478873    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/23

Mwanamuqawama
IQNA-Katika ajali mbaya ya helikopta iliyopelekea kuuawa shahidi Rais Ebrahim Raeisi, Iran pia ilimpoteza mwanadiplomasia mwanamapinduzi na shujaa ambaye aliingiza uhai mpya katika maisha ya sera kigeni za Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Habari ID: 3478870    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/22

Maombolezo ya Mashahidi
IQNA – Shughuli ya kuaga viwiliwili vya marehemu rais shahidi wa Iran Ebrahim Raisi, wenzake waliokufa shahidi aktika ajali ya helikopta imefanyika katika mji mtakatifu wa Qum mnamo Mei 21, 2024, kwa kushirikisha mamia ya maelfu ya watu.
Habari ID: 3478869    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/22

Maombolezo ya Mashahidi
IQNA - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas , Ismail Haniyah alipongeza misimamo ya marehemu rais wa Iran Shahidi Ebrahim Raisi ya kuunga mkono Palestina.
Habari ID: 3478868    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/22

Kuaga Mashahidi
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi ameswalisha swala ya maiti ya Shahidi Rais Ebrahim Raisi na mashahidi wenzake katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran.
Habari ID: 3478867    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/22

Maombolezo
IQNA – Shahidi Ayatullah Ebrahim Raisi alikuwa na shauku ya kuwatumikia watu, Rais wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) amesema.
Habari ID: 3478863    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/21

Maombolezo
IQNA - Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ametuma salamu za rambirambi kufuatia kufa shahidi Rais wa Iran Sayyid Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na ujumbe ulioandamana nao.
Habari ID: 3478862    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/21

IQNA - Bendera ya kijani kibichi ya Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS), Imam wa Nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia huko Mashhad ilibadilishwa na nyeusi kuashiria kuanza kwa siku tano za maombolezo ya kitaifa mnamo Mei 20, 2024, kufuatia vifo vya kusikitisha vya rais wa Iran, waziri wa mambo ya nje na ujumbe wa walioandamana nao katika ajali ya helikopta. Shahidi Raisi ni mwenyeji wa mji wa Mashhad na aliwahi wakati moja kuwa msimamizi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS).
Habari ID: 3478861    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/21

Maombolezo
IQNA - Idadi kubwa ya Wairani huko Tabriz wameshiriki katika shughuli ya kumuaga shahidi Rais Ebrahim Raisi na maafisa kadhaa waliokufa shahidi pamoja naye katika ajali mbaya ya helikopta iliyotokea Mei 19 milimani katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini-magharibi mwa Iran.
Habari ID: 3478859    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/21

Maombolezo
IQNA-Makundi ya mapambano ya Kiislamu (muqawama) katika eneo la Asia Magharibi yametuma salamu za rambirambi na kuonyesha mshikamano na taifa na serikali ya Iran kufuatia ajali ya helikopta jana ambayo helikopta ambayo ilipelekea kufa shahidi Seyyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje na wote waliokuwa katika msafaraha huo.
Habari ID: 3478857    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/20